Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Thursday, February 18, 2016

AFUKUZWA CCM AKIDAIWA KUMFANYIA KAMPENI LOWASA.

Geita. Halmashauri ya CCM Mkoa wa Geita imemvua ujumbe wa Mkutano Mkuu, Peter Mwininga baada ya kudaiwa kukiuka maadili ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Licha ya kukiuka maadili ya umoja huo, Mwininga anadaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita kwa kuwatukana viongozi wa ngazi za juu kwa njia ya mtandao.

Akizungumza baada ya kikao hicho juzi, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoani hapa, Said Kalidushi alisema baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kupokea malalamiko na mapendekezo kutoka UVCCM, waliamua kumvua nafasi ya ujumbe huo kutokana na kupungukiwa na sifa.

Kalidushi alisema wakati wa kampeni Mwininga alikihujumu chama chao na kumfanyia kampeni mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa, huku akijua wazi kuwa ni kosa.

Katibu wa UVCCM mkoani hapa, Mashaka Mshola alisema kitendo cha Mwininga kuvuliwa nafasi aliyokuwa nayo kinatokana na usaliti na huo ni mwanzo wa chama hicho kuwafukuza wasaliti

Read more »

Wednesday, February 17, 2016

Bodi ya Wazee Wa Chama Cha NRA Yasema Itashiriki Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar

Chama cha National Reconstruction Allience NRA kimewataka wanachama na wananchi kwa jumla kupuuza tamko la aliyekuwa mgombea wa Chama hicho kwa nafasi ya Urais, Seif Ally Idd kuwa yeye na chama wamejitoa katika marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Baraza la Wazee, Bodi ya chama na Kamati kuu ya Chama cha NRA msimamo wa kushiriki uchaguzi wa Zanzibar upo paleplae kama kikao cha kamati kuu cha Februari 6 mwaka huu kilivyoazimia.

Jijini Dar Es Salaam, Baraza la wazee na Kamati Kuu ya Chama cha NRA, Kimesema chama kitaendelea kushiriki uchaguzi kama kilivyodhamiria na kuwataka wanachama kushiriki uchaguzi huo kwa amani.

NRA Kimesema iwapo mgombea wa chama hicho Zanzibar amejitoa katika uchaguzi huo basi afuatae taratibu za kisheria kama alivyofuata taratibu za kugombea nafasi hiyo ya urais na sheria za chama.

Chama cha NRA kimesema katika nchi yoyote yenye Demokrasia, Uchaguzi ndiyo njia pekee ya kushika dola, NA kuwataka wananchi wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.

Chama cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea Urais katika uchaguzi wa Octoba 25, 2015, baadaye kufutwa kutokana na kasoro mbalimbali na ambao unatarajiwa kurudiwa tena Machi 20 mwaka huu.

Read more »

Thursday, December 3, 2015

MAMBO AMBAYO YALIVUMA NA KUFRAHISHA WENGI KABLA YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI DESEMBA 3/ 2015

  Nianze kwa kunukuu maneno ya kijana mwenye ulemavu na jasiri ambae kiukweli nimwite asiepende kucheza mbali na furusa pindi zinapompitia karibu nae ni aliekuwa mgombea uspika wa bunge la jamhuli ya muungano wa tanzania Bwana Peter Sarungi.


"Ndugu jamaa marafiki na wadau wangu wote na popote walipo, nitoe shukrani zangu za dhati kwa sappoti yenu toka nilivyoanza hatua ya kwenda kuwa spika wa bunge.



Ki ukweli nimefarijika sana na mapenzi yenu makubwa kwangu na kunichangia kwa hali na mali pamoja na ushauri mliokuwa mkinipa na kunifariji. 

Nilikwenda kushindana lakini pia nilikwenda kuzindua hatua zangu nyingi za mbele katika siasa.   
Nashukuru malengo yangu yamefanikiwa kwa 90% na huu ni ushindi kwangu kwa kuweza kufanikisha sauti yangu ya siasa kusikika kwa nchi nzima na kwa watawala wa nchi kwa mara ya kwanza."

Mimi nikiwa kama mtu mwenye ulemavu napenda sana kumpongeza bwana Sarungi kwa ujasili wa kutuwakirihsa vizuri watu wenye ulemavu na kutuondolea unyanyapa mabao ulikuwa bado umeganda kwenye baathi ya vichwa watanzania wakizani kuwa walemavu hawawawezi kumbe ndivyo sivyo, pia najuwa waliowengi wataungana nami bila kujali hali zetu za ulemavu kumpongeza Bwana sarungi.

Kwa kuzingatia maneno yako nndugu sarungi najuwa una malengo mengi sana ya kisiasa kama nilivyokunukuu napenda nimuombe mungu kwa niaba yako akupe moyo wa kujibidiisha katika kufikia malengo yako ambayo kiukweli yanafaida kwako na jamii nzima ya watu wenye ulemavu, kukosa uspika sio kukosa na mengine kaza buti na ukiwa unatambua kuwa mungu yupo pamoja na wewe kwa kila hatuwa. Amin




Read more »

Saturday, October 4, 2014

KILAINI! SITTA ANA MSONGO WA MAWAZO KITAIFA.


Dodoma. Sasa ni wazi kwamba Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta ameingia katika mgogoro na viongozi wa dini.

Wakati jana Sitta akirejea kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwamba waraka uliotolewa na viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania kuhusu mchakato wa Katiba kwamba "hauna utukufu wa Mungu na wa kipuuzi", viongozi hao wamesema mwanasiasa huyo ahurumiwe kwa kuwa "ana msongo wa mawazo".

Kauli ya Sitta

Sitta alisema nia ya baadhi ya viongozi hao wa dini ni kuliingiza Taifa katika machafuko, jambo ambalo alisema kama mtu mzima na mzee, hatalivumilia.

Waraka huo ulitolewa kwa pamoja na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (FPCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA).

Sitta alilieleza Bunge hilo kuwa lugha iliyotumika kuandika waraka huo aliokuwa nao na kusoma baadhi ya vipengele vyake, haina staha na haifai hata kidogo kutolewa na watu ambao wanahubiri dini na amani.

"Moja ya vitu ambavyo watu wanatakiwa kuviona, hivi wanaposema kuwa rais asimamishe mchakato wa Katiba, wanakuwa na maana gani? Hivi ni Ukristo huo kweli unaotokana na utukufu wa Mungu?" alihoji Sitta huku akishangiliwa na wajumbe. Alikwenda mbali akiifananisha lugha iliyotumika kuandaa waraka huo na ile aliyozoea kuisikia kutoka kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Akinukuu sehemu ya waraka huo iliyosema "mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba afanye kazi bila ya ubabe," alisema huo ni uongo kwani anafanya kazi kwa weledi mkubwa.

"Jamani, mimi ni Mkristo na wala sina ubabe wala kiburi. Hivi hawa wanaotutukana kule nje hawawaoni? maneno mangapi yanasemwa juu yetu na watu wale, hivi hii siyo siasa jamani? Waraka huo wa maaskofu umesomwa kila mahali na makanisani, unawezaje kusema Rais aifufue Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati tayari tume hiyo ilishajifufua yenyewe kwa kujibizana na Bunge kila wakati?"

Sitta aliendelea kueleza kuwa akiwa mzee na mtu mzima, atasimamia jambo hilo ,wanzo mwisho.


SOURCE: MWANANCHI.
Read more »

Friday, February 7, 2014

BUNGE LA KATIBA NDILO LINALOWEZA KUZIMA HOJA YA SERIKALI TATU.

CCM yapanga mikakati minne kuzima azma hiyo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeweka mikakati minne mikubwa kuhakikisha kinazima mapendekezo ya serikali tatu ili kubaki na mfumo wa serikali mbili ulioboreshwa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.


Msimamo huo wa serikali mbili umekolezwa zaidi juzi na hotuba ya mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM.

 Kikwete alisema sera ya CCM ni serikali mbili na akarejea kauli aliyopata kuitoa wakati wa hotuba yake ya kufunga mwaka kwamba mchakato wa katiba mpya ukivurugika, serikali itarudi kwenye katiba ya sasa ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa miaka yote.


Duru za siasa zinasema kuwa majina ya wajumbe kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yamekuwa magumu, kwani hayawezi kushawishika kukubaliana na sera ya CCM ya serikali mbili.
Kwa mujibu wa habari hizo, mkakati wa pili ni kupitia kikao maalumu cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM.

Habari zinasema kuwa kikao cha NEC kinatarajiwa kukutana siku chache kabla ya Bunge la Katiba ili kutoa msimamo wa chama kuhusu umuhimu wa serikali mbili na ubaya wa serikali tatu.

Kikao hicho ambacho ni mkakati wa pili, kinafuatiwa na mkakati wa tatu wa kuitisha kikao cha wabunge wote pamoja na wale wa Bunge Maalumu kuwaelezea namna ya kuzima mapendekezo ya serikali tatu.
Kikao hicho kitashirikisha wabunge wote, wabunge wa Bunge la Katiba kutoka nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi.

Habari zaidi zinasema kuwa mkakati wa nne upo kupitia kanuni za Bunge jipya la Katiba.

Inaelezwa kuwa upitishaji wa kanuni hizo utazingatia wingi wa kura za wabunge ambao unatoa nafasi kubwa kwa wabunge wa CCM kupitisha kanuni zitakazowasaidia kuzima hoja ya serikali tatu.

Duru za siasa ndani ya chama hicho tawala zinasema kuwa CCM haiko tayari kwa mfumo wa serikali tatu, kwani inaamini utavunja Muungano.


Mzozo wa muundo wa serikali tatu ulianza baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, chini ya Jaji Joseph Warioba, kuja na rasimu ya kwanza ambapo wananchi wengi walipendekeza mfumo wa serikali tatu.
Baada ya rasimu hiyo, CCM ilipitisha azimio na kulisambaza mikoani hadi ngazi ya chini na kuagiza mabaraza ya katiba yahakikishe yanatoa mapendekezo ya serikali mbili.

Pamoja na njama za CCM kutaka kuchakachua mapendekezo hayo, bado rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa kwa Rais Kikwete hivi karibuni, imekuja na mapendekezo ya serikali tatu, kinyume cha matarajio ya CCM.

Kutokana na hali hiyo, CCM inaamini sehemu pekee ya kubadilisha mapendekezo hayo ni kwenye Bunge la Katiba ambalo linatarajiwa kukutana wakati wowote mwezi huu.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2013, Bunge Maalumu la Katiba litakuwa na jumla ya wajumbe 635.


Read more »

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com