Monday, June 19, 2017

USEMAVYO MKATABA WA KIMATAIFA JUU YA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Kutokana na tukio la majuzi la kupigwa na kiteswa kwa watu wenye ulemavu nchini Tanzania wakidaiwa kufanya maandamo,  wakidai yako yao ya msingi iliyomo kwenye mkataba wa kimataifa IBARA YA 27 KIPENGERE CHA (f) “Kuendeleza ajira binafsi, fursa za biashara, ushirika na kuanzisha biashara;” na hii ni mahususi kwa watu wenye ulemavu pamoja ibara na vingere vingine vingi kama nilivyoviolozesha hapa chini.
Pia katika mkataba huu ni kwamba haujaacha kitu kwani umetowa majukumu mazuri na makubwa ya kutekerezwa kwa kila idara ya wizara na taasisi zote nini wajibu wao juu ya watu wenye ukemavu ikiwemo jeshi la police,  kinachonisikitisha ni kwamba elimu haijafika kwa wahusika hususani jeshi ka police nduo maana hawazinmtambuwa haki za wenye ulemavu kwa mjibu wa mkataba huu.
Mimi kama mwanaharakati natamani sana kila mtu atambuwe namna mkataba huu unavyosema ila nashindwa kuelewa mamlaka zinazohusika kwanini mpaka leo kuna watu au taasisi ambazo dhahili zimeonyesha kutombua na kufahamu mkataba huu unavyowataka kuwatendea watu wenye ulemavu,  na yote hii ni kwa sababu mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuufikisha na kusambaza elimu hii mhimu iliyosainiwa na serikali yetu chini ya MHE: RAIS DK JAKAYA MRISHO KIKWETE.  Mwaka 2009.

IBARA NA VIPENGERE VYA
MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA WATU WENYE UKEMAVU.

IBARA YA 1-- MADHUMUNI
Maafikiano haya yameandaliwa ili kuhakikisha kwamba:Watu wenye ulemavu ni pamoja na watu wenye vilema vya kudumu (mathalani: viungo, akili n.k) na wale ambao kwa sababu mbalimbali
hawajumuishwi katika jamii (mfano kutokana na vizuizi vya kimtazamo,
lugha, mazingira na sheria).

IBARA YA 11-- HALI YA HATALI NA DHARULA.
kutokana na majanga Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanalindwa wakati wa vita, majanga ya asili au
dharura nyinginezo.

IBARA YA 15 -- KUTOFANYIWA MATESO UKATILI AU KUDHALILISHWA.
1. Hakuna mtu atakayeteswa, kutendewa au kuadhibiwa katika hali ya kikatili au
kiudhalilishaji. Hakuna mtu atakayelazimishwa kushiriki katika majaribio ya kisayansi au kitabibu.

IBARA YA 16 -- KUTINYONYWA KUTOFANYIWA VURUGU AU KUNYANYASWA.
Nchi:
1. Zitapitisha sheria na kuchukua hatua
nyinginezo ili kuhakikisha kuwa watu wenye
ulemavu hawanyonywi au kudhalilishwa
wakiwa nyumbani au nje ya nyumbani.
2. Zitachukua hatua ya kuzuia udhalilishaji wa watu wenye ulemavu kwa kuwapa misaada na taarifa sahihi wao wenyewe
na familia zao.
3. Zitahakikisha kuwa sehemu na programu zinazowa-hudumia watu wenye ulemavu zinakaguliwa kila mara ili kudhibiti ukatili na manyanyaso

2. Nchi zinakubaliana,  kutunga sheria na kuchukua hatua nyingine ili kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu
wanalindwa dhidi ya mateso kama ilivyo kwa watu wengine.

IBARA YA 27 - KAZI NA AJIRA.
1. Watu wenye ulemavu wana haki ya kufanya kazi sawa na watu wengine;
wana haki ya kupata riziki kutokana na
kazi walizojiamulia kuzifanya katika
mazingira yaliyo wazi na yanayofikiwa na watu wote. Nchi zitatunga sheria na kuchukua hatua nyingi zinazofaa ili:
a) Kuondoa ubaguzi kwa misingi ya ulemavu katika maeneo yote ya ajira ikiwa ni
pamoja na katika hali ya kutafuta kazi, kuajiriwa kuendelea na ajira, kupandishwa cheo
kazini na kufanya kazi katika mazingira salama kiafya;
b) Kulinda ajira za watu wenye ulemavu kuhusu usawa katika malipo ya ujira kwa kazi
ile ile, usawa wa fursa, usalama kazini na uwezo wa kutoa malalamiko;
c) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kujiunga pamoja na kuingia
kwenye vyama vya wafanyakazi sawa na mtu mwingine yeyote;
d) Kuweka uwezekano wa watu wenye ulemavu kupata huduma za ushauri wa
mafunzo kazini.
e) Kupanua fursa za kazi, kuandishwa vyeo na kuwasaidia watu wenye ulemavu
kutafuta kazi na kudumu kazini;
f) Kuendeleza ajira binafsi, fursa za biashara, ushirika na kuanzisha biashara;
g) Kuajiri watu wenye ulemavu serikalini;
h) Kuhimiza na kuwasaidia waajiri kuajiri watu wenye ulemavu;
i) Kuwarahisishia watu wenye ulemavu kumudu kazi na mazingira yake kwa
kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika kwa ajili yao;
j) Kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata uzoefu wa kazi katika soko la ajira;
k) Kukuza programu zinazowasaidia watu wenye ulemavu kurudi kazini na kudumu na
ajira zao.
2. Nchi zitahakikisha kuwa watu wenye ulemavu hawafanywi watumwa/watwana. Nchi zitawalinda dhidi ya ajira za kushurutishwa sawa na wanavyolindwa watu wengine.

Mwisho naomba nisisitize kuwa KATIBA, SHERIA,  MATAMKO, NA MIKATABA mbalimbali ya kimataifa na kitaifa imetungwa ili itekerezwe na sio uvunjwe iweje leo serikali iliyosimamia na kuridhia mkataba huu inakuwa ya kwanza kuvunja mkataba huu? Sasa nini cha kufanya ili mkataba huu ili mateso,  manyanyaso ya namna kama hii ya wenye ulemavu kupigwa na kuteswa ikiwa ni pamoja na kusurubiwa ndani ya nchi yao yanakoma.
Pia utekelezaji wa thati wa mkataba huu ikiwa ni pamoja na mrejesho wa namna ya taifa au nchi mwanachama alivyotekeleza makubaliano ya mkataba huu yalivyofanyika nchini kitu ambacho sidhani kama kimefanyika na wahusika ya wenye ulemavu wakapewa au wakaona namna ya utekelezwaji ulivyofanikiwa.

Pia nawambea msamaha askari waliofanya kosa lile la kuwapiga wenye ulemavu kwa sababu naamini walikuwa hawajuwi mkataba huu unavyowataka kuwafanyia wenye ulemavu lakini niwatake asikali police na taasisi zingine mfatilie na kusoma mkataba huu ili yasijirudia kama yalivyotokea.  Asante kufatilia.

Source: correctnewstz.blogspot.com

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com