Nianze kwa kunukuu maneno ya
kijana mwenye ulemavu na jasiri ambae kiukweli nimwite asiepende kucheza mbali
na furusa pindi zinapompitia karibu nae ni aliekuwa mgombea uspika wa bunge la
jamhuli ya muungano wa tanzania Bwana Peter Sarungi.
"Ndugu jamaa marafiki na wadau
wangu wote na popote walipo, nitoe shukrani zangu za dhati kwa sappoti yenu
toka nilivyoanza hatua ya kwenda kuwa spika wa bunge.
Ki ukweli nimefarijika sana na mapenzi yenu makubwa kwangu na kunichangia kwa hali na mali pamoja na ushauri mliokuwa mkinipa na kunifariji.
Nilikwenda kushindana lakini pia nilikwenda kuzindua hatua zangu nyingi za mbele katika siasa.
Nashukuru malengo yangu yamefanikiwa kwa 90% na huu ni ushindi kwangu kwa kuweza kufanikisha sauti yangu ya siasa kusikika kwa nchi nzima na kwa watawala wa nchi kwa mara ya kwanza."
Mimi nikiwa kama mtu mwenye ulemavu napenda sana kumpongeza bwana Sarungi kwa ujasili wa kutuwakirihsa vizuri watu wenye ulemavu na kutuondolea unyanyapa mabao ulikuwa bado umeganda kwenye baathi ya vichwa watanzania wakizani kuwa walemavu hawawawezi kumbe ndivyo sivyo, pia najuwa waliowengi wataungana nami bila kujali hali zetu za ulemavu kumpongeza Bwana sarungi.
Kwa kuzingatia maneno yako nndugu sarungi najuwa una malengo mengi sana ya kisiasa kama nilivyokunukuu napenda nimuombe mungu kwa niaba yako akupe moyo wa kujibidiisha katika kufikia malengo yako ambayo kiukweli yanafaida kwako na jamii nzima ya watu wenye ulemavu, kukosa uspika sio kukosa na mengine kaza buti na ukiwa unatambua kuwa mungu yupo pamoja na wewe kwa kila hatuwa. Amin
0 comments: