Wednesday, February 17, 2016

Bodi ya Wazee Wa Chama Cha NRA Yasema Itashiriki Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Chama cha National Reconstruction Allience NRA kimewataka wanachama na wananchi kwa jumla kupuuza tamko la aliyekuwa mgombea wa Chama hicho kwa nafasi ya Urais, Seif Ally Idd kuwa yeye na chama wamejitoa katika marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Baraza la Wazee, Bodi ya chama na Kamati kuu ya Chama cha NRA msimamo wa kushiriki uchaguzi wa Zanzibar upo paleplae kama kikao cha kamati kuu cha Februari 6 mwaka huu kilivyoazimia.

Jijini Dar Es Salaam, Baraza la wazee na Kamati Kuu ya Chama cha NRA, Kimesema chama kitaendelea kushiriki uchaguzi kama kilivyodhamiria na kuwataka wanachama kushiriki uchaguzi huo kwa amani.

NRA Kimesema iwapo mgombea wa chama hicho Zanzibar amejitoa katika uchaguzi huo basi afuatae taratibu za kisheria kama alivyofuata taratibu za kugombea nafasi hiyo ya urais na sheria za chama.

Chama cha NRA kimesema katika nchi yoyote yenye Demokrasia, Uchaguzi ndiyo njia pekee ya kushika dola, NA kuwataka wananchi wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo.

Chama cha NRA ni miongoni mwa vyama 14 vilivyosimamisha wagombea Urais katika uchaguzi wa Octoba 25, 2015, baadaye kufutwa kutokana na kasoro mbalimbali na ambao unatarajiwa kurudiwa tena Machi 20 mwaka huu.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com