Read more »
Sunday, February 21, 2016
Friday, February 19, 2016
Today Jacqueline Mengi and Faraja Nyalandu Gave Us Corporate Chic Look Goals .
Faraja Nyalandu visited Jacqueline Mengi at her office and this is what they wore .
Faraja is wearing all white suit and Black pumps while Jacqueline is dressing up in a floral dress that went perfect with her Yellow shoes .
Read more »Wednesday, February 17, 2016
SERIKALI YAAGIZA VYOMBO VYA HABALI KUZINGATIA SHERIA ZA WATU WENYE ULEMAVU
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(HawapoPichani) kuhusu vyombo vya habari kutekeleza Sheria ya Watu wenye Ulemavu katika kupata habari.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Dkt Abdallah Possi (Aliyekaa) akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kwa kikao chake na vyombo vya habari leo ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (WatuwenyeUlemavu) Dkt Abdallah Possi ameviagiza vyombo vya habari nchini kuzingatia Sheria ya Watu wenye ulemavu kwa kuhabarisha kwa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu katika kutoa habari,
Akitoa agizo hilo mbele ya vyombo vya habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Waziri Possi amesema vyombo vya habari vinatakiwa kuwakumbuka na watu wenye ulemavu katika utoaji wa taarifa mbalimbali katika Magazeti, Radio naTelevisheni hasa kwa kuzingatia lugha za alama ambazo zitawawezesha kuelewa habari husika.
“ Naomba tubadilike wanahabari kwa kuwajali watu wenye ulemavu kwa kuwahabarisha na wao pia, nawataka wamiliki wa vyombo vya habari hususan Televisheni kuweka lugha za alama kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kupata habari mbalimbali zinazojiri katika taifa”
“Vyombo vya habari vinatakiwa kubadili uono wao juu ya walemavu na sio kwa kuangalia mambo hasi tu yahusiyo walemavu kwamba wana shinda,hawawezi, wanahitaji msaada ila pia kwakuangalia mafanikio yao katika kuleta maendeleo ya taifa kiujumla” Alisema Dkt Possi.
Aidha Dkt Abdallah Possi amewataka waandishi wa habari hasa wa magazeti kuzingatia lugha wanazotumia kandika habari za watu wenye ulemavu ili kuondoa fikra na dhana hasi na unyayapaa juu ya walemavu huku akitolea mfano baadhi ya lugha zinazotumika na baadhi ya waandishi katika kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu kuwa hazistahili.
Ametaja mfano wa lugha ambazo sio sahihi katika uandishi wa habari za wenye ulemavu mfano maneno vipofu, viziwi,vilema na maneno mengine bali wanatakiwa kutumia maneno yenye staa na yasiyoleta picha ya unyanyapaa na udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu ili kuondokana na dhana ya unyanyapaa na udhalilishaji wa watu wenye ulemavu.
Kupata habari ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria No 9 ya Mwaka 2010 inavitaka vyombo vya habari kuhabarisha watu bila kuwabagua watu wenye ulemavu, tuelewe kwamba pia watu wenye ulemavu wana haki ya kupata taarifa kama watu wengine.
Read more »TUNDU LISSU AHOJIWA NA POLISI KWA MDA WA SAA MOJA.
TUNDU LISSU NAYE AITWA POLISI KWA MAHOJIANO AHOJIWA KWA SAA MOJA
TUNDU Lissu, Mwanasheria wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia Mbunge wa Singida Magharibi leo jijini Dar es Salaam amehojiwa na Jeshi la Polisi kuhusu hoja alizozitoa kwenye Gazeti la MAWIO.
Lissu amehojiwa kwa zaidi ya saa moja Makao Makuu ya Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuhitajika kutoa maelezo kwa madai ya kutoa kauli za uchoelezwa zilizoandikwa kwenye Gazeti la MAWIO zilizohusu mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar.
Habari iliyoandikwa na gazeti hilo iliyobeba kichwa cha habari ‘Machafuko yaja Zanzibar’ inaelezwa kuwa sababu ya serikali kulifungia gazeti hilo tarehe 15 Januari mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kutoa maelezo Lissu amesema, serikali inajaribu kumziba mdomo asizungumzie kuhusu suluhu ya mgogoro wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar wakati wahusika hawazingatii misingi ya demokrasia.
“Wale waliobebwa kwenye uchaguzi leo wanataka kutufumba midomo tusizungumzie masula ya uchaguzi wa Zanzibar kwani machafuko yanaweza kutokea visiwani humo kwa tahadhari hiyo wanatuita wachochezi,” amesema Lissu.
Amesema kuwa, wao wametoa tahadhari ili yasitokee machafuko na umwagikaji wa damu na kwamba, Rais John Magufuli atawajibika kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kama alivyowajibishwa Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Amesema, mahojiano yake na Gazeti la Mawio ndio yaliyosababisha yeye kuitwa na kuhojiwa na polisi na kwamba, mtazamo wake ulioandikwa kwenye gazeti hilo ndio umechangia kufutwa kwa gazeti hilo.
Amesema kuwa hatokubali kuzibwa mdomo hata kama watatumia nguvu ya polisi.
Amesema, hatua ya Rais Magufuli kukakataa kujihusisha na mgogoro wa Zanzibar haikubaliki kwa kuwa ndiye ndiye atakayepeleka jeshi pale vurugu zitakapotokea.
Lissu amefika polisi hapo akiwa na mawakili wa watatu wa Chadema ambao ni Peter Kibatala, Fedrick Kiwelo na Hekima Mwasibu.
Amesema, baada ya mahojiano hayo polisi watapeleka jalada lake kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa hatua zaidi.
Read more »MHINDI AFUKUZWA KAZI KWA KUWAITA WAFANYAKZI MANYANI
Raia wa India, Dennis Smith ameachishwa kazi katika Hoteli ya Ramada kwa madai ya kuwatukana wafanyakazi wa ngazi za chini akiwaita nyani.
Smith, ambaye ni meneja wa chakula na vinywaji wa hoteli hiyo, aliwatukana na kuwadhalilisha wafanyakazi hao siku ya Sikukuu ya Wapendanao akiwatuhumu kushindwa kuandaa meza vizuri.
Kutokana na udhalilishaji huo, wafanyakazi wa hoteli hiyo jana waligoma wakishinikiza meneja huyo asimamishwe kazi au wao waache kazi.
Wakizungumza jana, baadhi ya wafanyakazi ambao waliomba majina yao yahifadhiwe walisema tabia ya meneja huyo imekuwa sugu na tukio la juzi lilikuwa halivumiliki. Walisema raia huyo wa India amekuwa mwenye majivuno na kutoa lugha chafu dhidi yao.
“Tumechoshwa, anatuitaje sisi nyani, hii tabia ni ya muda mrefu na sasa hatuwezi kuivumilia,” alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
Mwakilishi wa wafanyakazi hao, Mathew Misalaba alisema bosi huyo amekuwa akiwarushia maneno ya kuwadhalilisha kila wanapofanya makosa hata kidogo.
Alisema licha ya uongozi wa hoteli kuahidi kumsimamisha kazi Smith, wamelipeleka suala hilo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.
Meneja Rasilimaliwatu wa hoteli hiyo, Sebastian Nchimbi alisema tayari Smith ameachishwa kazi kutokana na tukio hilo.
“Tulizungumza na wafanyakazi wakatuambia kuwa hawataki Smith awepo kazini na sisi tukafanya uamuzi ili kuwalinda wafanyakazi wetu,” alisema.
Alisema waliamua kumwachisha kazi Smith baada ya kupata malalamiko mengi kutoka kwa wafanyakazi hao.
“Si tukio la mara ya kwanza na ndiyo maana tulipoona yamezidi tuliamua kuchukua hatua,” alisema.
Hata hivyo, Nchimbi alimsifu Smith akisema ni mtendaji mzuri na alikuwa na tija kwa hoteli hiyo ya kitalii lakini hakuwa na kauli nzuri kwa wafanyakazi Waafrika.
“Kiutendaji ni mzuri mno… yaani kwetu sisi tunapoteza mtu hasa, tatizo ni mdomo tu,” alisema.
Read more »Popular Posts
-
As wheelchair tennis grows in popularity and relevance in American sports, steps are being taken to introduce the sport in developing n...
Facebook
Twitter
RSS