Sunday, January 26, 2014

UJIO WA KIFIMBO CHA MALKIA WAWA KERO KWA VIONGOZI VYAMA.

Posted by Unknown  |  Tagged as: ,

Ujio wa kifimbo cha malkia chenye kuashiria kukalibia kuanza kwa mashindano ya Jumuia ya Madola ambayo hufanyika kila baada ya miaka
4 na inayotarajia kuanza mwezi Julay mwaka huu 2014 nchini Scotland.

Kiliwasili tanzania tarehe 18 na tarehe 19/01/2014, sherehe ya kukikimbiza ilianzia uwanja wa taifa na kupita katikati ya jiji la Dar es Salaam na  mnamo saa kumi ya jioni kiliwasili Ikulu kikiwa kimekusanya wanamichezo mbalimbali kama Para Olympic ngumi riadha, mieleka na mingine mingi sana, na kupokelewa na MHE: Rais, akiwa pamoja mkewe kipenzi cha roho yake mama salma kiwete.

Kero ya kifimbo kwa baadhi ya vionozi wa vyama vya michezo ilianzia pale Rais aliposimama na kuanza kuhutubia umati wa wana michezo na mabarozi waliokuwa katika viwanja vya ikulu { nanukuu maneno makali ya MHE: Rais aliyoyasema kwa kuwalenga viongozi ambao wamekuwa hawawajibiki iwapasavyo na hatimae kuanza kuilaumu serikali kuwa haiwapi misaada pindi timu ya taifa inapokuwa kambini kujiandaa na michezo mbalimbali.

KAULI YA RAIS KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO.
Mheshimiwa Rais bila kupoteza mda na kuficha mambo yanayofanywa na viongozi wa vyama vya michezo alisema, "serikali na hasa wizara imekuwa ikitupiwa lawama na vyama vya michezo kuwa haiwapi msaada wowote pindi timu ya taifa inapokuwa kambini kitu ambacho kimekuwa kikisababisha timu kutokufanya vizuri kwa sababu  ya kambi kuwa haina mda wa kutosha kukaa kambini kwa sababu tu! pesa zimekuwa hazitoshai kuweka kambi sehemu nzuri na kwa mda wa kutosha".

Rais alisema "kama kiongozi unaomba uongozi halafu unategemea serikali ikusaidia kuweka kambi sehemu nzuri na kwa mda wa kutosha bila wewe kama kiongozi ulieomba dhamana kwa wananchi ya kukiongoza chama kwa kuwapa ahadi kuwa wakikupa uongozi utafanya mengi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha timu ya  tanzania inakuwa inaweka kambi sehemu nzuri na kwa wakati na kuhakikisha tunaleta ushindani wa kutosha pamoja na kupata medali kila mashindano tutakayobahatika kushiriki, na huku wewe huonyehsi juhudi za jitihada zozote na kukalia kulalamika kuwa rais anapenda mpila wa miguu tu! mimi napenda michezo yote na  nyinyi ni mashahidi ila ninachosema viongozi acheni kuomba uongozi kwa lengo la kuongeza CV bila utendaji mzuri ambao utaishawishi serikalin na wadau wengine kuwapa sapoti, sio kukaa kila siku mnalalamika".

Rais alienda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa kenya kuwa, "hakuna mchezaji ambae ni maarufu na alieiletea sifa nchi ya kenya ambae ametokea mombasa, bali wengi wao wametokea mikoa ya lifti vale, kikuyu, nairobi, na mingineyo nje ya mkoa wa mombasa Rais alimaanisha kuwa kama kweli viongozi wanahitazi siku moja tanzania iondokane na kuitwa kichwa cha mwendawazimu ni lazima iige nchi za kenya na ethiopia kwa kuwatafta wakimbiaji wazuri kutoka mikoa ya SINGIDA, ARUSHA, MANYARA, NA NK  kwani hii ndio mikoa yenye hazina kubwa ya wachezaji wazuri ambao wataleta medali na ushindani, hii ndio siri ya wenzetu wakenya na waethiopia kuwa na mafanikio makubwa katika michezo na sisi tunaweza kuwa kama wao au kuwapita kama tutaamua kufanya kazi na kuacha kila siku kusema tanzania ina wakimbiaji wazuri wenye rekodi ambazo mpaka leo hazijavunjwa, watanzania hawataki kubaki na rekodi ya Bai pekee bali tunataka wakina bai na nyambui wengine nao wavunje recodi za wakina bai na nyambui kama wanavyofanya wakenya kwa kuzivunja recodi zao wenyewe kwa wenyewe" Mwisho wa kunukuu.

'Mimi nampongeza sana MHE: Rais kwa maneno yake mazuri na ambayo  yana faida na maana kubwa sana  kwa maendeleo ya michezo ya tanzania kama viongozi wetu watabadilika na kuamua kufanya kazi na kuwa na malengo ya kuleta maendeleo ya michezo hapa tanzania, kwa kuhakikisha kuna kuwa na michezo ya ndani ya mara kwa mara kutafta wachezaji kwenye mikoa kama alivyosema mhe; rais pia kuacha kuendekeza umimi na kuacha kualjai mahitaji mhimu ya timu ambayo tunahitaji ikatuletee medali kutuwakrisha vizuri, na mwisho sipendi kila siku kuona tanzania inaendelea kuwa na wachezaji waliofanya vizuri miaka 40 iliyopita bali nahitaji vijana wa karne hii ya 21 nao waonyeshe uwezo wao kwani uwezo wanao pia watanzania wanahitaji kuona timu ya taifa inaweka kambi sehemu nzuri na inayoendana na ehemu yanapofanyika mashindano sio mashindano yanafanyika makambako kwenye baridi nyuzi joto 19 halafu kambi inawekwa dar es salaam kwenye nyuzi joto 30, inatakiwa kwa kuwa makambako kuna bridi nyuzi joto 19 kambi iwekwe tunduma kwenye baridi nyuzi joto 12'.

NAKUPONGEZA SANA MHESHIMIWA RAIS KWA HOTUBA YAKO NZURI NA YENYE  UJUMBE MZULI NA MZITO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYAMA VYA MICHEZO, MUNGU AKUBALIKI SANA.



0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com