Thursday, January 30, 2014

MKENYA, KIPCHOGE KEINO! MW/KT KOC AWAFUNDA VIONGOZI WA VYAMA VYA MICHEZO WA TANZANIA.

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Kipchoge Keino! bingwa mara mbili wa Olympic  ni kama amewaambia viongozi wa RT chini ya mwenyekiti na katibu wake ambao wote kwa pamoja walisemwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa ni viongozi wanalalamika sana kuliko kuwajibika, pale Kipchoge alipowaambia wanariadha wa tanzania walioko kambini  Kenya  kuwa nguzo kuu ya kufanikiwa ni kuzingatia nidhamu, kujituma na kujiamini.

Keino ambae ni MW/KT wa KOC  aliipa tanzania nafasi mbili za wanariadha wake kuweka kambi  kenya maraa baada ya hivi kalibuni  kuwasili nchini kifimbo cha  Malkia chenye kuashiria  uzinduzi wa  michezo ya jumuiya ya maadola.

Akizungumzia hilo Keino alisema ''nimeamua kuwasaidia wakimbiaji wa Tanzania kutokana na mahusiano mazurri baina ya nchi hizo mbili katika masuara ya kimichezo'' na kuongeza kuwa ''kama wanariadha hao watafanya kile kinachowapeleka kwenye kambi hiyo watafika mbali''.

Kwa mujibu wa  Katibu mkuu wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui, wakimbiaji  Fadhil John  na willboard Peter ndio wamepewa nafasi hiyo na kuongeza kuwa wataondoka nchini wiki ijayo kwenda kenya kuanza kambi hiyo.

Mimi naona hakuna msaada mbaya ila naamini kuwa mtu akiamua kukupa msaada maana yake ameona unahitaji kupata msaada,  au  kwa maana harisi ni kuwa wewe huna uwezo wa kupata hicho kitu alichokusaidia, kwa maana hiyo mimi namshukuru sana Kipchoge kwa msaada wake mzuri na wenye faida kubwa kwa wanariadha wetu na kwa taifa letu pia, ila naomba viongozi wa RT kwa kama wamedhamini maada huu wa kipchoge basi naomba waonyeshe kuwa nao wanapenda wanamichezo wa tanzania hasa wanariadha kwa kuwapa kambi nzuri wanariadha waliobaki au watakaokuwa na kambi hapa Tanzania ili tujuwe kuwa nao wanamipango mizuri ya kuendeleza Riadha.

Pia sioni haja ya mpaka wakenya watoe msaada ambao sisi kama watanzania tunao uwezo wa kuwaweka wanariadha wetu kambini kwa mda wowote na sehemu yooyote endapo t! viongozi wetu wataamua kuwajibika kwa kufanya kazi kwa nia ya kuhakikisha Tanzania inakuwa na wanariadha wazuri na ambao wataenda kuleta medali,  NAKUPONGEZA SANA KIPCHOGE KWA KUSAIDIA KAMBI WANARIADHA WETU NA HII IWE CHACHU YA KUAMKA KWA VIONGOZI WETU WA MICHEZO.

SOURCE: MWANANCHI

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com