Wednesday, December 31, 2014

TUTAKUKUMBUKA DAIMA MAMA PAULINA KILENZA MZAZI WA DEO NA PROVIAN DANDI

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Naomba nianze kwa kumshukuru mungu kwa kila jambo yeye ni yote katika yote, watu wengi tunaonekana kutumia muda mdogo
kufikiria kuhusu mauti; au kuhusu desturi zetu
wenyewe, ambazo ni sababu kubwa za mauti.


Kukosa hivi kujihoji nafsi kunaongoza kukosa
maarifa ya wenyewe, na kwa sababu hii watu huchukuliwa kufuata maisha, tukifanya maamuzi yetu kulingana na tunavyoamriwa na haja ya miili yetu.

Kupo kukataa ingawa kwa ukubwa
kumefichwa - kuchukuliwa ukweli wa kwamba
uhai ni mfupi mno hata watu wote pia hali ya
mwisho ya mauti itakuwa juu yetu.'Uzima wenu ni
nini ?  Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa
kitambo, kisha hutoweka’ "Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyowezekana kuzoleka tena"
"Asubuhi huwa kama
majani yameayo: asubuhi yachipuka (Ujana wetu)
na kumea, jioni yakatika na kukauka" (Yakobo
4:14; 2 Sam.14:4; Zab. 90: 5,6). Musa kweli mtu wa
kuhubiri, alitambua hili, alimwomba Mungu: "Basi,
tufundishe - tujulishe kuzihesabu siku zetu, ili
tujipatie moyo wa hekima" (Zab. 90:12) . Basi, kwa
mtazamo wa ufupi wa maisha, tendo la kupata
hekima ya kweli tutalipa kipaumbele.

Kuvutika kwa mtu na Mauti kwa hali ya mwisho ni
kwa namna nyingi. 

Mila nyingine zimejaribu
kufanya mauti na maziko ni sehemu ya maisha,
hupunguza maana ya msiba na kuwa hali ya
mwisho. Hao wengi wachukuao jina la "Kristo"
Wamedhani, kuwa mtu anayo'Roho - nafsi
isiyokufa’ au kitu fulani kinachoishi milele ndani
yake kinachopona mauti; kinaendelea kuishi
sehemu nyingine zaidi na jambo liletalo huzuni kwa
mwanadamu, itegemewe ya kwamba moyo wa mtu
umezoezwa sana kupunguza mgongano wa akili
yake; kwa hiyo shabaha yote ya nadharia potovu
imetokea kuhusu mauti na desturi hasa za mtu.
Kama siku zote, hizi inabidi zipimwe dhidi ya
Biblia ili kupata ukweli kuhusu hili jambo muhimu
la kuzungumuziwa. Ikumbukwe kuwa uongo kabisa
wa kwanza ulioandikwa ndani ya Biblia ni ule wa
nyoka katika bustani ya Edeni. Tofauti na taarifa
kamili ya Mungu kuwa mtu "hakika atakufa" kama
akitenda dhambi ( Mwa. 2:17) . nyoka alidai,
"Hakika ninyi hamtakufa" (Mwa. 3:4) . Uongo huu
unajaribu kukana hali ya kufikia mwisho kwa kufa
kabisa hivi imekuwa ni desturi ya dini zote potovu,
ni dhahiri hasa kwa eneo hili, fundisho moja la
uongo laongoza lingine, lingine na lingine. kwa
kinyume, neno moja la kweli laongoza lingine,
kama lilivyoonyeshwa na 1 Kor. 15:13 -17 . Hapa
Paulo anaruka toka ukweli mmoja hadi mwingine
(angalia "Kama ….Kama …. Kama….").
Kuelewa desturi zetu kweli, tunatakiwa kuona
Biblia yasemaje kuhusu Uumbaji wa mtu. Taarifa
imo katika lugha ya wazi, ambayo, ikichukuliwa
kama ilivyo, hatuwi na mashaka hasa kuhusiana na
mwili ulivyo (tazama kitambo kinachozungumziwa
sehemu ya 18 kuhusu maneno yalivyo katika kitabu
cha Mwanzo). "BWANA Mungu akafanya mtu kwa
mavumbi ya ardhi …. Katika hiyo (ardhi) ulitwaliwa
( Wewe Adamu) kwa maana u mavumbi wewe nawe
mavunbini utarudi" (Mwa. 2:7; 3:19). Hapa hakuna
kidokezo kabisa kuwa mtu yeyote amerithi kitu
kisicho kufa; hakuna sehemu iliyo ndani yake
inayoendelea kuwa hai baada ya kufa.
Upo mkazo wa Biblia ulioonyeshwa juu ya ukweli
kwamba mtu kwa ukubwa ametokana na mavumbi
tu: "Sisi tu Udongo" (Isa. 64:8) ; "Mtu wa kwanza
atoka katika nchi, ni wa udongo" (1Kor. 15:47) ; Mtu
msingi wake ni katika mavumbi" (Ayu. 4:19) ; "mtu
hurejea tena kuwa mavumbi" (Ayu. 34:14,15) .
Abrahamu alikiri kwamba alikuwa "ni mavumbi na
majivu tu" (Mwa. 18:27) .Mara baada ya kuvunja
amri ya Mungu pale Edeni, Mungu akamfukuza
huyo mtu ….. asije akanyoosha mkono wake,
akatwaa matunda ya mti wa uzima , akala, akaishi
milele" (Mwa. 3:24,22) . ikiwa mtu alikuwa na kitu
kisichokufa kwa kawaida ndani yake, hii amri
isingekuwa ya lazima kumzuia.

MWISHO SINA LA ZIADA ZAIDI YA KUUNGANA NA FAMILIA YA MAREHEMU KWA KIPINDI HIKI CHA MSIBA WA MAMA YETU KIPENZI PAULINA,

PIA NAOMBA NDUGU JAMAA TUUNGANE KWA PAMOJA KUMWOMBA MUNGU AMLAZE MAMA YETU PAULLINA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com