Sunday, January 4, 2015

MALINZI ATEULIWA TENA KUWA MWENYEKITI WA BMT

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia amesema Dioniz Malinzi ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nkamia alisema Malinzi ataendelea kuwa mwenyekiti wa BMT kwa miaka mingine mitatu.

“Serikali imeridhia Malinzi aendelee kuwa mwenyekiti wa BMT baada ya kuonyesha utendaji mzuri katika kipindi cha miaka mitatu aliyoliongoza baraza hilo,” alisema Nkamia na kueleza kuwa atasaidiana na wajumbe 10 sambamba na makatibu wakuu wa vyama vya michezo.

Malinzi alisema hajapewa taarifa rasmi ingawa kama Serikali imeridhia aendelee kuongoza BMT, yuko tayari kufanya hivyo.

Malinzi atafanya kazi na wajumbe, Zainabu Vullu, Crescentius Magori, Alex Mgongolwa, Zainabu Mbiro, Jennifer Shang’a, John Ndumbaro, Jamal Rwambo, Zacharia Hanspoppe, Mohamed Bawazir na Adam Mayingu.

BMT ipo kwa ajili ya kusimamia vyama vya michezo na kuhakikisha kupitia vyama hivyo michezo inapiga hatua na kufuata taratibu za kikanuni kama ambavyo katiba ya kila chama inavyosema.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com