Friday, March 28, 2014

WATU WASIO NA ULEMAVU WAWATUMIA WALEMAVU KUJINUFAISHA WAO WENYEWE! BAADA YA KUWASAIDIA.

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Chama cha Walemvu VICOBA Dar es salaam (WAVIDA)kimemlalamikia rais wa Vicoba Tanzania,Devota Likokola kwa madai ya kutowapatia fedha zilizotolewa na mwenyekiti wa IPP,Dkt.Reginald Mengi kwa ajili ya kikundi hicho.  

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Mwenyekiti wa Vicoba ilala,Joyce Robi alisema kuwa fedha hizo kiasi cha sh.milioni 100 waliahidiwa na Dkt.Mengi lakini cha kushangaza fedha hizo zimo mikononi mwa Likokola.


Alisema kuwa,Dkt.Mengi aliwapa ahadi hiyo mwaka 2012 baada ya kutembelea kikundi chao na kujionea shughuli wanazozifanya na kuvutiwa na hivyo alitoa ahadi hiyo kwa lengo la kuwasaidia ili wasonge mbele zaidi na hatimaye kuwasaidia wenzao wenye ulemavu.


"Lakini cha kushangaza zaidi fedha hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Devota Likokola kitu ambacho sijaelewa kuwa kuna nini kati ya Mengi na Likokola,"alisema Robi.
Alisema kuwa,fedha hizo zimesababisha kikundi hicho kugawanyika na baadhi ya watu kuhama huku wakiwa na madeni ya kulipa kwenye kikundi hicho.


Aliongeza kuwa,walipokuwa wakitafuta ufafanuzi kutoka kwa mtoa fedha hizo walikosa kwani walipokuwa wakifika ofisini kwake walimkosa hivyo kuwa na wasiwasi juu ya fedha hizo.


"Kitendo hicho cha fedha kwenda moja kwa moja kwenda kwa Mheshimiwa Likokola kimesababisha wanachama wetu kutuona sisi viongozi wao kama wezi na hata wengine kuhama kikundi na kujiunga na vikundi vingine alisema Robi.


Naye Katibu wa kikundi hicho,Seif Mohamed alisema kuwa kikundi kilikuwa na wanachama 150 lakini mpaka sasa wamebaki wanachama 120 huku wengine wakiwa wamekopa na kuondoka na fedha
"Hutujui kuwa kuna ajenda gani kati ya Mengi na Likokola hadi fedha hizo ziingizwe kwenye akaunti ya Likokola"alisema Mohamed.


"Napenda kuwaasa wenzetu wote wenye ulemavu kutokubali kutumika na watu kwani baadhi ya wamekuwa wakiwatumia kwa lengo la kujinufaisha wao",alisema.
Alisema kuwa,wanachotaka ni Dkt.Mengi kutoa tamko kuwa fedha hizo zinamhusu Likokola au kikundi hicho cha Vicoba Ilala ili waweze kufahamu.



MHE: Devota Likokola, Mbunge viti maalum Ruvuma

 Wakiongea kwa ,asikitiko makubwa sana kwa kitendo alicholifanya MHE: Likokola ambae sio mlemavu na ambae hana huruma kabisa kwa kutumia cheo chake cha Uenyekiti wa VICOBA Tanzania japo sio mwenyekiti wa vyama vyote vya VICOBA na kwenda kuchukuwa pesa kwa Mwenyekit wa makampuni ya IPP  kwa kudai atawafikishia  walengwa na matokeo yake asifikishe na kuamua kubaki nayo, 

 Pia wanachama hawa walilalamika zaidi kwa kitendo cha MHE: Likokola cha kuligawa kundi kwa kuamuwa kuwachukuwa baathi ya wanachama na kuwagawia pesa hizo akiamini kuwa itakuwa kinga kwake kwa siku za baadae lakini wanachama hawa wakasema wao wanajuwa mbinu hii aliyoitumia n wao hatakubaliana hadi hapo hali yao na msaada wao utakapojulikana mwisho wake.



 

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com