Mnamo tarehe 20/03/2014 Serikali ya Tanzania kupitia mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ilitangaza Oparesheni ya kuzuia Bajaj, maguta, Bodaboda, na Maloli, kufisa katika ya jiji kwa madai yasio na sababu za msingi, tena bila kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu pia bila kujali wala kujiuliza kuwa kuwazuia walemavu wasiingia katikati ya jiji na kuwawekea mpaka kuwa mwisho sehemu flani ni sawa na kumwambia mtu asie mlemavu kuwa tumia miguu yako lakini usifike sehemu flani kitu ambacho ni cha ajabu na cha kushangaza sana, na ambacho hakijawahi kufanya na nchi yoyote Duniani.
Kwa uelewa wangu mdogo naamini kuwa kila Serikali au Taasisi inapotaka kufanya kitu au maamuzi yoyote lazima iweke makundi maalum kwenye mjadala ili pindi watakapotoa maamuzi, maamuzi yasije yakawaumiza watu wenye Ulemavu na ni utaratibu unafanya popote pale penye makundi maalum kama ilivyo kwenye usafili wa Bajaj Jijini Dar es salaam.
Pia nasikitika kuwa ni serikali hii hii ndio hutoa vipaumbele kwa watu wenye ulemavu wkati wa kupiga kula wakipita kutangaza kwa vipaza sauti na kwenye vyombo vya habali kuwa "ndugu watanzania tuwa ndugu watanzania tunapenda kuwatangazia kuwa wakati wa kupiga kula tuwapishe watu wenye ulemavu waende mbele na wasipange foleni na wakati mwingi tunawekewa msitali wetu,
je? huruma ile huwa ya kinafiki na kama sio ya kinafiki kwanini istumike na wakati huu hasa kwenye swara hili la bajaj kuzuiliwa kuingia mjini?
naomba mtambuwe kuwa Bajaji kwa watu wenye ulemavu ni miguu yao hivyo haiwezekani mkaiwekea mipaka kwa hili haliwezekani, toka lini mguu wa mtu ukawekewa mpaka?
 |
Baazi ya bajaj za watu wenye ulemavu zilizokamatwa na majembe kwa agizo la Sumatra.
ikiwa Rais wetu wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania alisaini Mkataba huu wenye kuheshimu maswala ya watu wenye ulemavu kama unavyomeka
''Ibara ya 17
Kuheshimu tofauti za kimaumbile
Kila mtu mwenye ulemavu anayo haki ya kuheshimiwa kwa ukamilifu
wake kimwili na kiakili kwa misingi ya usawa na watu wengine.
Ibara ya 18
Uhuru wa mtu kwenda atakapo na kuwa na utaifa
1. Waliouridhia
Mkataba huu wanatambua haki za watu wenye ulemavu za
kuwa huru kwenda popote watakapo, uhuru wa kuchagua makazi yao na utaifa kwa
misingi iliyo sawa na watu wengine.''
Je/ kwanini walemavu wa Tanzania hatusaminiwi kama mkataba wa Kimataifa unavyosema?
''Ibara ya 20
Matembezi binafsi
Waliouridhia Mkataba huu watachukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa watu
wenye ulemavu wanajitegemea kwa kadri inavyowezekana katika kumudu kutembea
ikiwa ni pamoja na:
(a) Kumwezesha
mtu binafsi mwenye ulemavu kutembea kwa namna na wakati anaotaka mwenyewe na
kwa gharama atakayoimudu;''.
|
|
|
|
|
0 comments: