Thursday, April 30, 2015

Babaake Kim Kardashian sasa ni mwanamke

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Bruce Jenner aliyekuwa mwariadha bora duaniani kabla
ya kuwa nyota wa kipindi cha televisheni na familia
moja maarufu duniani ''The Kardashians''. sasa amefichua siri ambayo amekuwa akiificha kwa miakamingi.


''Kwa nia na madhumuni yote, mimi ni mwanamke.''
Jenner aliambia Sawyer kutoka ABC katika mahojiano
maalum yaliopeperushwa hewani siku ya Ijumaa.


''Watu wananiona tofauti,wananiona kama mwanaume,
lakini moyo na roho yangu na kila kitu ninachofanya
maishani ni sehemu yangu.'' Jenner ambaye ana umri
wa miaka 65 amesema. '' Upande huu wa kike ni
sehemu yangu.


hivi ndivyo mimi nilivyo.''
Bruce Jenner
Katika masaa ya mahojiano na Diane Sawyer mjini New
York na California, Jenner alielezea kwa kina
mapambano yake ya kuwa na jinsia mbili tangu utotoni.


''Akili zangu ni za kike sana kuliko za kiume.''
Ameongezea. '' Ni vigumu sana watu kuelewa, lakini
hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyo.''
Jenner aliyejawa na hisia na mwenye nywele ndefu
shati na suruali ndefu alisema kuwa amesubiri kwa
miaka mingi ili kujitangaza kwa kuwa hakutaka
kuwavunja moyo watu.


Kwa miongo kadhaa wake wa zamani wa Jenner na
madada zake waliweka siri kuhusu jinsia yake na
kwamba walikuwa watu waliokuwa wakijua siri hiyo.


Mtandao wa watu wanaojua siri hiyo hatahivyo
ulipanuka hivi majuzi wakati Jenner alipomwambia
mamaake na wanawe 10 .


Jenner ana watoto sita
Burt,Cassandra,Brabdon,Brody,Kendall na Kylie pamoja
na watoto wanne wa kambo akiwemo
Kourtney,Kim,Khloe na Rob Kardashian.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com