Wednesday, February 4, 2015

Zitto aikaba koo Serikali mapato ya Tanzanite soko la nje

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe leo imeikaba koo Serikali na kutaka itoe majibu ya kina kuhusu mapato yatokanayo na mauzo ya madini ya Tanzanite katika soko la nje.

Katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma, Zitto aliomba muongozo wa Spika mbele ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu akidai kuwa majibu yaliyotolewa na Serikali katika swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Kidawa Hamid Salehe (CCM) yalikuwa mepesi na hayakujibu kabisa swali hilo.

Awali Kidawa aliuliza swali bungeni hapo akitaka kujua kiasi gani cha mapato kitokanacho na mauzo ya Tanzanite katika pato la taifa katika kipindi cha 2011 hadi 2014.

Mbunge huyo pia alihoji ni kiasi gani cha fedha kimepotea kutokana na vito vya Tanzanite kwa kuuzwa kwa njia isiyo halali katika kipindi cha 2011 – 2014.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Mwijage alisema katika kipindi cha 2011 hadi 2014 kiasi cha Sh 5.92 bilioni kiliingizwa katika pato la Taifa kama mrahaba.

“Mwaka 2011 zilikuwa Sh 1.24 bilioni, 2012 zikapatikana 1.53 bilioni, wakati mwaka 2013 zilifikia bilioni 1.67 na mwaka 2014 zikawa Sh 1.48 bilioni,” alisema Mwijage.

Kuhusu kiasi kilichopotea alitaja kuwa ni dola 400 milioni kupitia nchi za Kenya na India na kwamba wanunuzi wakuu wa Tanzanite duniani ni Marekani, India, Hong Kong, Jamhuri ya Afrika Kusini, Sri-Lanka na Thailand.

Hata hivyo majibu hayo hayakumridhisha Zitto na hivyo kuomba muongozo akitaka swali hilo lijibiwe upya na kwa kina kwani majibu ya naibu waziri yalikosa utashi katika kulinda madini ya Tanzanite.

Mwenyekiti wa Bunge aliridhia muongozo huo na kutaka wizara kuja na majibu yanayostahili.

SOURCE: mwananchi.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com