Sunday, February 15, 2015

TANZANIA PARALYMPIC WAPATA VIONGOZI WAPYA.

Posted by Unknown  |  Tagged as:

GWAKISA PAUL MWAKABETA
Ameukwaa Urais wa Chama cha michezo ya watu wenye Ulemavu ( Paralympic) kwenye uchaguzi mkuu wa viongozi  uliofanyika jana kwenye ukumbi wa jwahi la wokovu na kusimamiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Mwakabeta amechukuwa nafasi ya johnson jason alietumikia kwa kipindi cha miaka tisa 9, na hivyo kuamua kutogombea kwa awamu nyingine.

Mwakabeta amewashinda wagombea wengine wengine watatu akiongoza kwa kura 18, Ain Sharifu, aliepata kura nne 4, Hamadi Abdallah Komboza alipata kura 0, John Ndumbaru alipata kura 10,.

                NAFASI YA MAKAMU WA RAIS.
alieshinda nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais ni Samwel Kafyeta na Tuma Dand ambae ni mwandishi katika kutuo cha mlimani wagombea hao hawakuwa na wapinzani.

                  NAFASI YA KATIBU
Katika nafasi ya Katibu mkuu aliwashinda aliekuwa ni Peter Sarungi aliepata kura 20 akiwashinda aliekuwa Katibu mkuu aliepita Idd Kibwana aliepata kura 9, na Moses Mabula aliepata kura tatu 3.

                  NAFASI YA MHASIBU.
Wagombea walikuwa watatu na matokeo ni Honorina Banzi amewashinda alipata kura 22, akiwashinda alikuwa mhasibu aliepita Yusuph poss aliepata kura nane 8, na Alex alipata kura 2.

               WAJUMBE KAMATI YA UTENDAJI.
Wagombea walikuwa kumi na sita16,  Na washindi  saba 7 ambao ndio wamekuwa wajumbe wa kamati ya utendaji ni mchezaji wa Tennis Yohana mwila, alipata kura 23, Zaharan mwenemti, kura 23,  Ally Kiponda, Said Malilo, Hamza Waritu, Shaban Shomary, na Ernest Nyabalale.

akizungumza mara baada ya uchaguzi Katibu mkuu wa BMT Henry Rihaya aliueleza.uongozi mpya kuwa moja ya mambo mhimu ambayo yantakiwa kufanyiwa mrekebisho haraka sana ni katiba ya TPC  kwani haiko vizuri na pia nawapa siku 90, kuanzia leo hii na ifikapo mwezi wa tani tarehe kama ya leo kama sio katiba tuone hata rasim ya katibu.

0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com