Thursday, February 5, 2015

AZAM YAJIVUNIA MAFANIKIO WALIYOYAPATA CONGO

Posted by Unknown  |  Tagged as:

Licha ya kushindwa kushinda mechi hata moja katika kambi iliyoweka katika Jamhuri ya watu wa Kongo (DRC), mabingwa wa soka Tanzania Bara , Azam FC wamesema kuwa ziara hiyo ilikuwa na mafanikio katika maandalizi yao ya mechi ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya vigogo wa Sudan, El-Merreikh.

Msemaji wa Azam, Jaffar Idd ameiambia BBC Dar es Salaam kuwa wamepata mazoezi ya kutosha licha ya kutoshinda.

“Tumejua makosa yetu na udhaifu wetu, kocha tayari amerekebisha na tupo tayari na mechi yetu dhidi ya El-Merreikh”, alisema Iddi.

Azam imerejea Dar es Salaam leo (Alhamisi) ikitoka Lubumbashi na baada ya kurudi wanajiandaa na mechi kadhaa za ligi kuu ya Tanzania kama maandalizi yake ya mwisho kabla kuwavaa Wasudan.

Wakiwa Sudan, walicheza na mabingwa mara nne wa ligi ya mabingwa Afrika, klabu ya TP Mazembe na kufungwa 1-0.

Pia walitoka droo ya 2-2 na timu ya Zesco na kufungwa 1-0 na Don Bosco katika mechi yao ya mwisho.

Iddi amesema wana matumaini makubwa ya kuanza vyema michuano ya kimataifa baada kuyafanyia kazi mambo kadhaa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Azam kushiriki michuano hii ya ligi ya mabingwa Afrika na itacheza na El Merreikh ya Sudan Februari 15 jijini Dar es Salaam. Mechi ya marudiano itachezwa Khartoum, Sudan baada ya wiki mbili.

Wawakilishi wengine wa Tanzania Bara ni Yanga ikipangiwa kuanza na Botswana Defence Force (BDF) ya Botswana katika Kombe la Shirikisho.

Kwa upande wa Tanzania Visiwani, Polisi ya Zanzibar itacheza na CF Mounana ya Gabon katika Kombe la Shirikisho huku KMKM ikipangiwa kucheza na Al Hilal ya Sudan katika Ligi ya Mabingwa Afrika


0 comments:

Popular Posts

Author

Yohana Mwila

Translator

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
Copyright © 2013 CORRECT NEWSTZ BLOG. Powered by Blogger.
Blogger Template by Bloggertheme9
+255 (784) 033-443yohanamwila@gmail.com