Kwanza naomba tutambuwe michezo sio
mpira wa miguu tu! Bali ni michezo yote kama Riatha, Tennis, kurusha Tufe,
kurusha Kisahani, Kuogelea, Mpira wa Magongo, Tebo Tennis, Ngumi, Netball,
Handball, na michezo hii kwa nchi nilizozita
hushirikisha watu wenye walemavu na wasio na ulemavu, kwa kuwa lengo la taifa
lolote lenye nia ya kulitangaza taifa lake na kutaka kupata medali kupitia
michezo huwa halishuguliki na mpira wa miguu tu! Bali na michezo mingine.
Kwa mfano nchi za wenzetu kama Kenya,
Uganda, Ethiopia, Rwanda, South Africa, na zinginezo hazifanyi vizuri sana
kwenye mpira wa miguu, lakini kwenye michezo mingine mataifa yao yanajulikana
sana Duniani kupitia michezo mingine ambayo sisi Tanzania hatutaki kuipa
kipaumbele.
Jamaniwatanzania wenzangu kama soka
imeshindikana tutowe furusa na kwenye michezo mingine sisi kama watanzania
wenye uchungu na Taifa letu ambalo lina hamu sana ya siku moja tuanze kereta
medali kama mvua na hatimae JINA la Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu
Lisiwepo na lisije kuendelea kutajwa tena kwani ni aibu kwa taifa lenye vipaji
rukuki sana vya wachezaji wa kila aina ya mchezo
Na Siku zote nimekuwa nikisema ukweli na sitaweza
kusifia kitu ambacho hakistahili sifa yoyote sioni sababu ya kusema safi kama
sio safi sioni sababu ya kusema ndiyo kama jibu ni hapana siwezi sema one
wakati ni ziro, Zaidi ya kucema kuwa serikali na watendaji wake tuanhane na
mpira wa miguu unatuchelewesha kupata medali na kujulikana Duniani kwa kuwa Tanzania ni nchi ina kila sababu ya
kufikia zaidi ya walipo majirani zetu na wasio majirani zetu kwani tuna vipaji
vya kila aina, nasema ni Ujinga kuendelea kufanya Biashara inayokutia hasara
kila siku.
TFF mnayo majibu juu ya
kwanini soka letu halina radha , tukianza na ligi zetu bado hazijaonyesha sura
ya kwamba siku moja timu yetu ya taifa itacheza soka lenye mvuto
ukitazama soka la leo pale taifa ni wazi kuwa mchezo wa timu yetu umekuwa
ni mchezo wa mchezaji mmoja mmoja sijaona soka la timu sijaona mchezo wa kitimu
maana sijaona hata kama mabadiliko yanayoweza
kubadili mchezo nimeona wazi kukosekana kwa fulani mchezo wa timu nzima unabadilika.
Natoa ushauri kwa TOC na TPC na kama
hamtasoma hapa basi nawaomba wanachama wa TOC ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu wakipata nafasi ya kuchangia
katika mikutano yenu naomba wanisemee yafuatayo ..
- Ipo haja ya kuangalia upya jinsi gani ya mashindano yetu ya taifa ambayo ndio yanayoweza kuvumbua vipaji, waangalie jinsi mfumo unaotumika kuendesha mashindano haya mhimu, kama uendeshwaji wake unakizi viwango na vigezo.
- Maboresho katika usimamizi wa Timu za Taifa za vijana zinapokuwa kambini na kwenye maandalizi ya aina yeyote kama hayana kaoro na kama yana kasoro basi kasoro hizo zirekebishwe bila kumwangalia mtu usoni, na bila kumwogopa mtu kwa aina yake awe savimbi, marehemu gadafi, marehemu hosama bini ladeni au kwa vyovyote atakavyokuwa kwa kuwatanzania au nafasi anayoishikiria hajajipa mwenyewe bali nyinyi wajumbe kwa kutuwakrisha watanzania tulio wengi ndio mmewapa.
- Kusuka upya timu za taifa ambazo zitatafutiwa michezo mingi ya kirafiki na ikiwezekana tukasimama kushiriki mashindano ya kimataifa hata kwa miaka miwili .
Na kwako msomaji unaweza ongezea
mengine unayodhani yanafaa ili tusiendelee kuwa kichwa cha mwehu...
Ingia
hapo TUMA MAONI ili uweze kuongezea ya kwako
Captean:
yohana mwila.
www.yohanamwila.blogspot.com
0 comments: